Kikao hicho ambacho kinafanyika chini ya anwani ya “Mchango wa Dini katika Maisha ya Mtu Binafsi na Jamii” kinasimamiwa na Kituo cha Mazungumzo kati ya Dini Mbalimbali na kanisa la Orthodox la Russia.
Kikao hicho kimeanza kwa kiraa ya Qur’ani na Injili na kufunguliwa kwa hotuba ya Hujjatul Islamu Malaki, Naibu Mkuu wa Kitengo cha Utafiti na Elimu cha Jumuiya ya Utamaduni na Mawasiliano ya Kiislamu ya Iran.
Masuala muhimu yaliyojadiliwa katika kikao cha leo ni mchango wa dini katika maisha ya mtu binafsi na jamii, nafasi ya dini katika kuboresha mahusiano ya kijamii na uhuru, haki na dini katika mtazamo wa madhehebu ya Orthodox.
Vilevile hadhirina walijadili maudhui za ada za Kiothodox na haki za binadamu na nafasi ya dini katika kustawisha thamani za kimaadili.
Kikao hicho kitakamilisha kazi zake kesho. 669670