Kijitabu hicho cha kurasa 72 ni chenye thamani kubwa kwa watu walio na hamu ya kujua shughuli za kifedha na mfumo wa benki wa Kiislamu.
Robert Aini, mkurugenzi mwandamizi wa Jumuiya ya Mfumo wa Benki wa Bahrain amesema kuwa kijitabu hicho kimeandikwa kwa lugha nyepesi ambayo inafahamika na hata watu wasiokuwa wataalamu wa masuala ya benki na shughuli za kifedha za Kiislamu.
Kwa kutumia mafundisho na sheria za Kiislamu kuhusiana na masuala ya fedha na biashara, mfumo wa benki wa Kiislamu ulifanikiwa kukwepa na kutoathirika kwa njia yoyote ile na mgogoro wa fedha uliozikumba nchi nyingi za Magharibi hivi karibuni, jambo linalothibitisha wazi kwamba mfumo huo una uwezo mkubwa wa kuvutia uwekezaji zaidi wa Waislamu ulimwenguni.
Inasemekana kuwa Bahrain ndiyo nchi iliyo na benki na taasisi nyingi zaidi za kifedha za Kiislamu katika eneo la Mashariki ya Kati, na kuchapishwa kijitabu hicho bila shaka ni hatua muhimu katika uwanja wa kuwapasha habari zaidi za kifedha watu walio na hamu ya kunufaika na mfumo huo wa Kiislamu kuhusiana na masuala ya kifedha na kibenki. 669549