IQNA

Italia kuwa mwenyeji wa maonyesho ya kimataifa ya 'Sanaa katika Utamaduni wa Kiislamu'

15:24 - October 11, 2010
Habari ID: 2010796
Maonyesho ya tatu ya kimataifa ya 'Sanaa katika Utamaduni wa Kiislamu' yatafanyika tarehe 19 Oktoba katika mji wa Milan nchini Italia.
Ufunguzi wa maonyesho hayo utahudhuriwa na Mawaziri wa Habari na Mafuta wa Kuwait, Meya wa Milan, wanafikra na wanadiplomasia wa ulimwengu wa Kiislamu.
Vitu vitakavyoonyeshwa katika maonyesho hayo ya kimataifa baadaye zitapelekwa na kuonyeshwa katika majumba ya makumbusho ya baadhi ya nchi duniani.
Maonyesho ya kwanza ya athari za sanaa za Kiislamu za Kituo cha Athari za Kiislamu cha Kuwait yalifanyika mwaka 1990 katika mji wa Saint Petersburg nchini Russia. 672576


captcha