IQNA

Tamasha la kuwaenzi mahafidhi wa Qur'ani kufanyika Jiddah

15:12 - October 13, 2010
Habari ID: 2012372
Tamasha ya 31 ya kuwaenzi mahafidhi wa Qur'ani Tukufu na wanafunzi wa Jumuiya ya Masuala ya Kheri ya Kuhifadhi Qur'ani itafanyika tarehe 17 katika mji wa Jiddah nchini Saudi Arabia.
Tamasha hiyo itafanyika katika hoteli ya Hilton Jiddah ikihudhuriwa na viongozi wa Jumuiya ya Masuala ya Kheri ya Kuhifadhi Qur'ani, wanafunzi wa taasisi hiyo na mahafidhi wa Qur'ani nchini Saudi Arabia.
Mkuu wa jumuiya hiyo Abdul Aziz bin Abdullah Hanafi amesema kuwa katika miaka ya hivi karibuni jumuiya hiyo imepiga hatua kubwa katika nyanja za elimu na mafunzo.
Amesema kuwa Jumuiya ya Masuala ya Kheri ya Kuhifadhi Qur'ani ya Jiddah inafanya juhudi za kutoa mafunzo ya Qur'ani kwa watu wa matabaka yote ya jamii.
Ameongeza kuwa jumuiya hiyo daima imekuwa ikifanya jitihada za kuanzisha masomo ya kuhifadhi Qur'ani kwa vijana wa kike na kiume na kuwahamasisha kwa ajili ya kutekeleza mafundisho ya kitabu hicho kitukufu. 674264


captcha