Kwa mujibu wa gazeti la nchi hiyo la al-Qabas, hafla ya kuarifishwa washindi hao ilihudhuriwa na Rashid al-Hammad, Waziri wa Wakfu na Masuala ya Kiislamu wa Kuwait pamoja na Naibu Waziri Mkuu wa Kuwait anayeshughulikia masuala ya kisheria.
Washindani 3166 walishiriki katika hatua ya mwanzo ya mashindano hayo ambapo mwishoni washiriki 1667 walichaguliwa kushiriki katika hatua ya mwisho ya mashindano hayo. Hatimaye washiriki 153 walichaguliwa kuwa washindi wa mwisho wa mashindano hayo ambayo yaliwashirikisha wanawake na wanaume.
Othman as-Sha'lan alitangazwa kuwa mshindi wa kwanza katika kundi la wanaume waliohifadhi Qur'ani nzima na alitunukiwa zawadi ya dinari 3000 za Kuwait.
Katika kundi la wanawake, Intiswar as-Swuleihim alitangazwa kuwa mshindi ambapo pia alitunukiwa zawadi hiyohiyo ya dinari 3000.
Katika hafla hiyo Waziri wa Wakfu na Masuala ya Kiislamu wa Kuwait alisema kuwa kushiriki vijana katika mashindano hayo ni njia bora zaidi ya kuwakinga na vitisho pamoja na changamoto za kifikra zinazowakabili katika zama hizi na kuwashawishi waendelee kuzingatia zaidi mafundisho ya Qur'ani maishani. 675280