IQNA

Iran katika maonyesho ya Kiutamaduni na Kielimu ya Zimbabwe

15:46 - October 18, 2010
Habari ID: 2015202
Maonyesho ya kiutamaduni, kielimu na kisanaa ya 'Victoria Falls' ya Zimbabwe yamefanyika katika mji mkuu wa nchi hiyo Harare na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imeshiriki kwa upana katika maonyesho hayo.
Kwa mujibu kitengo cha IQNA katika Shirika la Utamaduni na Mahusiano ya Kiislamu ICRO, Idara ya Utamaduni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mjini Harare imewasilisha vitabu vya kitaalamu kuhusu Uislamu na Iran mbali na kuwasilisha sanaa za mikono na bidhaa nyingine za utamaduni za Iran katika maonyesho hayo.
Maonyesho hayo ambayo yamefanyika katika kituo kikubwa zaidi cha mafunzo katika mji huo yamehudhuriwa na jumuiya za kiraia, jumuiya za wanawake na vijana, taasisi za teknolojia ya mawasiliano na vile vile taasisi za elimu.
Mwambata wa Utamaduni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Zimbabwe Bw. Mohammad Asadi Muwahid amehutubia hadhara ya watu 1,300 katika maonyesho hayo. Katika hotuba yake ameashiria historia ya Iran kabla na baada ya Uislamu.
Mwishoni mwa hotuba yake amejibu maswali ya hadhirina kuhusu Uislamu, Qur'ani Tukufu na Ukristo kwa mtazamo wa Uislamu. Aidha amefafanua kuhusu ustawi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran licha ya vikwazo vya Marekani na madola ya Magharibi.
676978
captcha