Mwambata wa Utamaduni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Uingereza Ali Mohammad Hilmi ametembelea kitengo cha masomo ya Asia na Mashariki ya Kati katika Chuo Kikuu cha Cambridge na kuhudhuria maonyesho ya 'Hamasa ya Wafalme wa Iran, Sanaa ya Shahname ya Ferdowsi'.
Kwa mujibu kitengo cha IQNA katika Shirika la Utamaduni na Mahusiano ya Kiislamu ICRO, Helimi amekutana na mhadhiri mwandamizi wa lugha ya Kifarsi Profesa Charles Melville na kujadili masuala yanayohusu ufundishaji wa lugha ya Kifarsi na masomo ya Kiirani katika Chuo Kikuu cha Cambridge.
Maonyesho ya 'Hamasa ya Wafalme wa Iran, Sanaa ya Shahname ya Ferdowsi' yanafanyika kwa mnasaba wa kumbukumbu ya mwaka wa 1000 wa kuandika Shahname ya Ferdowsi.
Maonyesho hayo ni natija ya utafiti mkubwa kuhusu Shahname uliofanywa na watafiti na wasomi katika uga wa Iran ulioanza mwaka 1999 katika Chuo Kikuu cha Cambridge.
676105