Kwa himaya ya Idara ya Utamaduni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mjini Istanbul, mafunzo ya majira ya mapukutiko ya ukalimani wa lugha ya Kifarsi yanatolewa katika kituo cha Jumuiya ya Waandishi wa Uturuki kitengo cha Istanbul.
Kwa mujibu kitengo cha IQNA katika Shirika la Utamaduni na Mahusiano ya Kiislamu ICRO, Bw. Muqtaderi mtaalamu wa masuala ya utamaduni na mkuu wa Idara ya Utamaduni ya Iran mjini Istanbul ameishukuru Jumuiya ya Waandishi wa Uturuki kitengo cha Istanbul kwa kuchangia katika masomo hayo.
Amesema 'mkalimani mwenye uwezo ni yule aliye na ujuzi wa lugha na tamaduni za lugha mbili anazotumia, hii ni kwa sababu mkalimani anasambaza fasihi, utamaduni na maarifa ya taifa moja hadi taifa jingine'.
Duru hiyo ya masomo inawajumuisha wanachuo 12 wa lugha ya Kifarsi na wapendao kazi ya ukalimani.
Washiriki watajifunza mbinu na maarifa ya ukalimani kutoka lugha ya Kifarsi hadi lugha ya Kituruki cha Istanbuli.
676072