Dharau ya nchi za Magharibi dhidi ya kitabu kitakatifu cha Qur'ani imechunguzwa katika toleo jipya la 326 la jarida la Kiarabu la al-Wahda linalojadili masuala ya kidini, kisiasa, kiutamaduni na kijamii.
Jarida hilo ambalo hutolewa mara moja kila baada ya mwezi mmoja na kusambazwa katika zaidi ya nchi 120, linazungumzia katika kurasa zake za mwanzo, suala la Qud Tukufu na kuadhimishwa kwa kishindo Siku ya Kimataifa ya Quds katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Suala la pili lililopewa umuhimu na jarida hilo ni kukosewa heshima kitabu kitakatifu cha Qur'ani huko nchini Marekani na nchi nyingine za Ulaya na ujumbe mkali uliotolewa na Ayatullahil Udhma Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran kuhusu jambo hilo. Ayatullah Khamenei alisema katika ujumbe huo kwamba lengo la dharau hiyo dhidi ya matukufu ya Kiislamu ni kuzusha woga na hofu dhidi ya Waislamu katika nchi za Magharibi. Jarida hilo linazungumzia kwa urefu radiamali iliyotolewa katika pembe mbalibali za dunia dhidi ya hatua ya Kasisi Terry Jones wa jimbo la Florida nchini Marekani ya kutaka kuchomwa moto Qur'ani Tukufu. Mahojiano ya Rais Mahmoud Ahmadinejad wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na televisheni ya al-Jazeera, nafasi ya harakati ya Hizbullah ya Lebanon katika kuzuia vita vya kieneo katika Mashariki ya Kati, suala la Afghanistan, mazungumzo batili eti ya amani ya Mamlaka ya Ndani ya Palestina na Wazayuni na maandishi ya marehemu Allama Muhammad Hussein Fadhlullah kuhusiana na umaraja' ni masuala mengine muhimu yaliyoakisiwa katika jarida hilo. 678275