IQNA

Maonyesho ya Kimataifa ya 'Sanaa katika Utamaduni wa Kiislamu Italia

18:35 - October 20, 2010
Habari ID: 2016643
Maonyesho ya tatu ya kimataifa ya taasisi za athari za Kiislamu za sanaa Kuwait imeandaa maonyesho ya 'Sanaa Katika Utamaduni wa Kiislamu' yaliyoanza Oktoba 19 katika mji wa Milan nchini Italia.
Kwa mujibu wa Shirika rasmi la habari la Kuwait KUNA, sherehe za ufunguzi wa maonyesho hayo zimehudhuriwa na al Salim al Sabah Mkaguzi Mkuu wa taasisi za athari za Kiislamu za sanaa nchini Kuwait, Jabir Duaij al Ibrahim la Sabah Balozi wa Kuwait nchini Italia, Meya wa Milan, Sheikh Ahmad Al Abdullah Al Sabah Waziri wa Habari na Mafuta wa Kuwait, Balozi wa Italia nchini Kuwait na wasomi wa Kuwati na wanadiplomasia wa nchi za Kiislamu nchini Italia.
Maonyesho hayo yana athari za sanaa za Kiislamu na sanaa za mkono za Kiislamu na yana lengo la kuarifisha thamani za utamaduni wa Kiislamu kwa Wamagharibi. Maonyesho hayo yataendelea hadi wiki ya kwanza ya mwezi Februari mwakani.
678920
captcha