Gazeti la New York Post limeripoti kuwa kazi hizo za kisanii ambazo baadhi yao zinarejea kipindi cha miaka 1500 iliyopita, zinaonyeshwa kwa ajili ya kudhihirisha masuala yanayokutanisha pamoja dini hizo tatu.
Mkuu wa maktaba kuu ya New York amesema kuwa maonyesho hayo ambayo yanasisitiza juu ya masuala yanayozikutanisha pamoja dini tatu za Uislamu, Ukristo na Uyahudi yataanza Ijumaa ya tarehe 22 Oktoba.
Amesema kuwa maonyesho hayo yataendelea hadi tarehe 27 Februari. Ameongeza kuwa kati ya kazi 200 za kisanii zinazoonyeshwa kwenye maonyesho hayo imo nakala na kale zaidi ya Qur'ani Tukufu. 679193