Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, maonyesho hayo yanajumuisha zaidi ya Qur'ani Tukufu 200 zilizoandikwa kwa hati za mkono, Taurati, Injili na vitabu vyenye itibari vya kidini vya Wakatoliki, Waorthodoxi, Waprotestanti na Waislamu.
Wakuu wa Maktaba ya Kitaifa ya Marekani wameashiria kuwa wafuasi wa dini hizo tatu wanatoka katika kizazi cha Nabii Ibrahim (AS) na kusema kuwa, Waislamu, Wakristo na Mayahudi waliishi pamoja katika karne zilizopita na kwamba maisha haya ya amani yangali yanaendelea huko New York. Misahafu ya kale kutoka nchi za China, Morocco, Iran, Iraq, Uturuki, Bulgaria na Misri na vile vile vitabu kuhusu Miraji ya Mtume SAW na taratibu ya kufanya ibada ya hija ni kati ya athari zilizo katika maonyesho hayo.
Maonyesho hayo ya 'Uislamu, Ukristo na Uyahudi' yanatazamiwa kuendelea kwa muda wa miezi minne. 679944