IQNA

Maonyesho ya picha za 'Misikiti ya Morocco katika Historia' yaanza

9:58 - October 24, 2010
Habari ID: 2018057
Maonyesho ya picha yenye maudhui ya 'Misikiti ya Morocco Katika Historia' imeanza Ijumaa tarehe 22 Oktoba katika mji wa Casablanca.
Kwa mujibu wa tovuti ya casafree, maonyesho hayo yalifunguliwa rasmi na Mfalme wa Morocco Mohammad wa Sita katika hafla iliyohudhuriwa pia na Waziri wa Masuala ya Kiislamu nchini humo.
Maonyesho hayo yanajumuisha athari 70 bora za mpiga picha maarufu Abduladam Peter Sunders wa Uingereza ambaye amepiga picha misikiti mbalimbali ya Morocco na turathi maarufu za usanifu majengo nchini humo. Aidha katika maonyesho haya kitabu kuhusu 'Misikiti ya Morocco katika Historia' kilichoandikwa na Abdul Hariri kimezinduliwa. 680756
captcha