IQNA

Juhudi za Mawahabi za kuzuia kuadhimishwa Siku ya Hadhrat Ali Asghar (as)

11:53 - October 24, 2010
Habari ID: 2018450
Wazayuni na Mawahabi wanafanya juhudi kubwa za kuzuia kuadhimishwa siku ya kumuenzi Hadhrat Ali Asghar (as), na hilo linatokana na kuenea kwa kasi athari za siku hiyo duniani.
Akizungumzia suala hilo katika kikao cha nne cha wasimamizi wanaoandaa hafla hiyo, Abdul Adhim al-Muhtada al-Bahrani, mwanaharakati na mwandishi wa Bahrain amesema Mawahabi na Wazayuni wamekuwa wakifanya juhudi kubwa za kuzuia kuandaliwa kwa mafanikio Siku ya Kimataifa ya Hadhrat Ali Ashghar (as). Ametaka kuitwa siku hiyo kuwa Siku ya Kimataifa ya Shahid na kutaka kila juhudi na suhula za lazima zitumike kwa ajili ya kuifanikisha.
Amesema, siku hiyo inapasa kuchukuliwa kuwa utangulizi wa kudhihiri Imam wa Zama, Imam Mahdi (af).
Tunakumbusha hapa kuwa Siku ya Kimataifa ya Hadhrat Ali Asghar (as) huandaliwa na Jumuiya ya Kimataifa ya Kumuenzi Hadhrat Ali (as) katika Ijumaa ya kwanza ya mwezi wa Muharram. 680788
captcha