IQNA

Maonyesho ya "Sanaa ya Kaligrafia ya Kiislamu' Munich

12:06 - October 25, 2010
Habari ID: 2019271
Maonyesho ya Kimataifa ya "Sanaa ya Kaligrafia ya Kiislamu" yameanza wiki hii katika mji wa Munich nchini Ujerumani na yanatazamiwa kuendelea hadi mwezi Februari mwakani.
Kwa mujibu wa gazeti la Uturuki la Hurriyet, maonyesho haya yamefunguliwa rasmi katika hafla iliyohuduriwa na Mkuu wa Jumba la Makumbusho la Staatliches Claudius Muller na wakuu wa ubalozi wa Uturuki nchini Ujerumani.
Akizungumza katika sherehe za ufunguzi Muller amesema, 'maonyesho ya athari za Kiislamu Munich yalianza mwaka 1910 na kwamba mwaka huu maonyesho hayo yanafanyika kuadhimisha mwaka wa 100 tangu kuanzishwa.
681899
captcha