IQNA

Jumba la Makumbusho la Sanaa za Kiislamu lafunguliwa Cairo

17:20 - October 25, 2010
Habari ID: 2019438
Jumba la Makumbusho la Sanaa za Kiislamu limefunguliwa Jumatatu Oktoba 25 mjini Cario .
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, Katibu Mkuu wa Baraza Kuu la Athari za Kale la Misri amesema, 'Jumba la Makumbusho ya Sanaa za Kiislamu ndio jumba kubwa zaidi la makumbusho la sanaa za Kiislamu duniani'. Ameongeza kuwa athari za sanaa zilizokusanywa hapo zinaashiria vipindi mbalimbali vya mabadiliko ya sanaa ya Kiislamu katika Ulimwengu wa Kiislamu.
Amesema athari za sanaa za Jumba la Makumbusho ya Sanaa za Kiislamu la Cairo zinajumuisha hati, vyombo vya chuma,mawe ya kale, sanaa za mikono, seramiki, pembe za ndovu na sarafu za kale za Misri na nchi mbalimbali za Kiislamu. 682116

captcha