IQNA

Kikao cha 'Wajibu wa Waislamu Mbele ya Qur'ani' kufanyika Ufaransa

17:32 - October 25, 2010
Habari ID: 2019580
Kikao cha Wajibu wa Waislamu Mbele ya Qur'ani Tukufu kimepangwa kufanyika Jumamosi ijayo chini ya usimamizi wa msikiti wa Boundy nchini Ufaransa.
Kikao hicho kitafanyika baada ya swala ya Magharibi kikihudhuriwa na Sulaiman Shamal ambaye ni miongoni mwa viongozi wa taasisi ya uchapishaji ya Avant l'Heure ya Ufaransa na Waislamu wa mji wa Boundy ulioko katika vitongoji vya Paris.
Kikao hicho kitajadili maudhui mbalimbali ikiwa ni pamoja na umuhimu wa Qur'ani katika maisha ya Waislamu, mbinu za kufundisha kitabu hicho cha Mwenyezi Mungu na njia za kueneza mafundisho yake.
Watu wote wanakaribishwa kushiriki katika kikao hicho ambacho pia kitakuwa na sehemu ya maswali na majibu. 682227
captcha