IQNA

Tunisia, mwenyeji wa warsha ya Sura ya Wanawake wa Kiislamu katika Vipindi vya Redio

13:15 - October 26, 2010
Habari ID: 2020125
Warsha ya kieneo itakayojadili Sura ya Wanawake katika Vipindi vya Redio za Nchi za Waislamu za kaskazini mwa Afrika inaanza leo Jumanne nchini Tunisia na kuendelea kwa kipindi cha siku tatu.
Warsha hiyo inasimamiwa na Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Jumuiya ya Nchi za Kiislamu ISESCO likishirikiana na Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa UNESCO.
Lengo la washa hiyo limetajwa kuwa ni kuchunguza hali ya sasa ya sura ya wanawake katika vipindi vya redio za eneo la kaskazini mwa Afrika na kufanya jitihada za kuboresha suala hilo, kuwaelimisha wanaharakati wa kike wanaofanya kazi katika vyombo vya habari na kutumia mbinu za kisayansi kwa ajili ya kubadili sura isiyokuwa sahihi ya wanawake katika baadhi ya vipindi vya redio.
Warsha hiyo inahudhuriwa na wanaharakati wa sekta ya vyombo vya habari vya sauti na televisheni kutoka nchi za Tunisia, Algeria, Morocco, Mauritania na wataalamu wa UNESCO, Mfuko wa Ustawi wa Wanawake wa Umoja wa Matafa (UNIFEM), Jumuiya ya Kuwazindua Wanawake ya Kauthar na Wakala wa Ushirikiano wa Tunisia na Ujerumani. 682822

captcha