Shirika la Sayansi, Elimu na Utamaduni la Umoja wa Mataifa UNESCO limewatumia barua viongozi wa utawala wa Kizayuni wa Israel likipinga hatua ya kuorodheshwa maeneo matakatifu ya Kiislamu huko Palestina katika turathi za kiutamaduni za Mayahudi.
UNESCO imesema katika barua hiyo kwamba matukufu ya Kiislamu ya Palestina ni sehemu ya turathi za Waislamu na limepinga vikali kuorodheshwa katika turathi za Wayahudi.
Barua hiyo ya UNESCO imekaribishwa na Jumuiya ya Wanafikra na Walinganiaji wa Kiislamu wa Palestina. Jumuiya hiyo imetangaza kuwa barua hiyo inayoyaondoa maeneo ya Msikiti wa Nabii Ibrahim na Msikiti wa Bilal bin Ribah na katika turathi za Kiyahudi ni hatua inayopaswa kupongezwa.
Taarifa ya jumuiya hiyo imeongeza kuwa utawala wa Kizayuni wa Israel unaharibu athari na matukufu ya Kiislamu katika mji wa Quds na umebadilisha baadhi ya maeneo na athari za Kiislamu za mji huo.
Taarifa ya Jumuiya ya Wasomi na Kiislamu wa Palestina imeitaka UNESCO kufuatilia uharibifu unaofanywa na utawala ghasibu wa Israel katika mji wa Quds na kufanya juhudi za kuusimamisha. 686663