IQNA

Nahjul Balagha yafasiriwa kwa Kifaransa

11:20 - November 04, 2010
Habari ID: 2025349
Kitabu Nahjul Balagha kimefasiriwa kikamilifu kwa mara ya kwanza kwa lugha ya Kifaransa.
Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawzah, Mkuu wa Shirika la Kimataifa wa Nahjul Balagha Ayatullah Sayyed Jamaluddin Dinparvar, mpango wa tafsiri hiyo umekuwepo kwa miaka 30 sasa.
Amesema mwanamke Muislamu Mfaransa Hassina Ahmad bin Abdurrahman ametekeleza jukumu nzito la kuifasiri Nahjul Balagha kwa Kifaransa. Ayatullah Dinparvar amesema Nahjul Balagha imefasiriwa kwa zaidi ya lugha 20 na kuongeza kuwa, kwa ushirikiano wa Shirika la Utamaduni na Uhusiano wa Kiislamu kuna mpango wa kufasiri kitabu hicho kwa lugha zingine 12.
Nahjul Balagha ni mjumuiko wa hotuba, barua na semi za Imam Ali bin Abi Twalib AS. Kitabu hicho kilikusanywa na Sayyid Radhi zaidi ya miaka elfu moja iliyopita. Kitabu cha Nahjul Balagha kinahesabiwa kuwa hazina ya kipekee ya fasihi na maarifa ya Kiislamu.
687896
captcha