Maonyesho hayo yametayarishwa na Chama cha Wachapishaji wa Vitabu Tanzania (PATA) kwa ushirikiano wa Baraza la Maendeleo ya Vitabu Tanzania” (BAMVITA).
Maonyesho hayo yametayarishwa kwa lengo la kustawisha utamaduni wa kusoma vitabu katika jamii. Wachapishwaji Tanzania, wawakilishi wa nchi kadhaa za Afrika Mashariki na wachapisaji wa kimataifa watashiriki katika maonyesho hayo.
Idara ya Utamaduni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imepanga kuonyesha vitabu vya kidini na kijamii, majarida na vile vile CD/DVD kwa lugha za Kiarabu, Kiswahili na Kiingereza.
688873