IQNA

Mkutano wa ISESCO kuhusu jamii za Waislamu wachache kufanyika Rabat

15:12 - November 06, 2010
Habari ID: 2026398
Mkutano wa 11 wa Baraza Kuu la Elimu, Sayansi na Utamaduni kwa ajili ya jamii za Waislamu waliowachache katika nchi mbalimbali umepangwa kufanyika mjini Rabat, Morocco.
Mkutano huo utafanyika tarehe 8 Novemba ukisimamiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Jumuiya ya Nchi za Kiislamu ISESCO Abdul Aziz Othman al Tuwaijri.
Mkutano huo utajadili na kuchunguza ripoti ya shirika la ISESCO kuhusu shughuli zake katika fremu ya stratijia za kiutamaduni na Kiislamu kwa ajili ya Waislamu wanaoishi nje ya ulimwengu wa Kiislamu, mipango ya ISESCO ya kutayarisha waandishi habari katika taasisi za kipropaganda za Kiislamu barani Ulaya kwa ajili ya kujibu hujuma za vyombo vya habari dhidi ya Uislamu na ustaarabu wake na mpango wa stratijia ya kustawisha elimu katika shule za Kiarabu na Kiislamu nje ya ulimwengu wa Kiislamu.
Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Jumuiya ya Nchi za Kiislamu ISESCO mwaka 2001 lilianzisha Baraza Kuu la Elimu, Sayansi na Utamaduni kwa ajili ya Waislamu wanaosihi katika jamii zisizokuwa za Kiislamu ikiwa ni sehemu ya stratijia ya harakati za kiutamaduni na Kiislamu kwa ajili ya Waislamu wanaoishi nje ya ulimwengu wa Kiislamu. 689089
captcha