Kikao cha kila mwaka cha waku wa misafara ya hija ya nchi za Ulaya, Marekani, Australia na Uturuki wamekutana katika mji Mtakatifu wa Makka.
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, mkutano huo umeitishwa kujadili kuhusu namna ya uratibu wa ibada ya hija miongoni mwa wakaazi wa nchi za Magharibi.
Reza bin Rashad Ajemi Mkuu wa Idara ya Uratibu wa Mahujaji Barani Ulaya amesema kikao hicho kimefanyika ili kujadili njia za kuratibu ibada ya hija na kuhakikisha mahujaji wa nchi hizo wanatekeleza ibada ya hija kwa ipasavyo na kwa nidhamu.
Ameongeza kuwa wakuu wa misafara ya hija ya Ulaya, Uturuki, Marekani na Australia watatumia mbinu kadhaa kuongoza mahujaji wa nchi hizo ikiwa ni pamoja na ujumbe mfupi wa simu za mkononi, utawanyaji vijitabu kwa lugha mbalimbali ili kuhakikisha ibada ya hija inatekelezwa kama ilivyopangwa. 689357