Ali Tamim Mwenyekiti wa Baraza la Idara la Msikiti wa Sheikh Zayid amesema kuwa nakala hizo za Qur'ani tukufu zina umri wa miaka 500 na zilitawanywa barani Ulaya kati ya mwaka 1537 na 1857 Miladia.
Amesema kuwa maktaba hiyo ina nakala zenye thamani kubwa za Qur'ani zilizoandikwa kwa hati za mkono, vitabu adimu na nyaraka zenye thamani kubwa. Ameongeza kuwa vitabu vya maktaba hiyo vinahusu maudhui mbalimbali za kisayansi na kiutamaduni na vimeandikwa kwa lugha 12 za dunia. 691061