Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Pakistan, maonyesho hayo yalijumuisha athari za kaligrafia ya Kiislamu za wasanii mashuhuri wa Palestina na vilevile wasanii chipukizi.
Jumba la Makumbsho la Lok Virsa hivi karibuni liliwaalika wasanii mashuhuri wa Pakistan kuonyesha athari zao na vilevile kushiriki katika mashindano ya kaligrafia.
Karibu wanakaligrafia 25 mashuhuri wa Pakistan walishiriki katika maonyesho na mashindano hayo. Majaji wa mashindano ya kaligrafia ya Jumba la Makumbsho la Lok Virsa walijumuisha mabingwa wa fani hiyo nchini Pakistan.
Wenye athari sita bora za kaligrafia walitunukiwa nishani na taasisi hiyo katika hafla iliyohudhuriwa na waziri wa utamaduni wa Pakistan. 691422