Ofisi ya Ayatullah Sayyid Ali Sistani, Marjaa wa Waislamu wa madhehebu ya Shia imetangaza kuwa tarehe 8 Novemba itakuwa siku ya kwanza ya mwezi wa Dhul Hija na kwa hivyo sikukuu ya Idul Adh'ha itakuwa tarehe 17 Novemba.
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, Ofisi ya Ayatullah Sistani imetoa taarifa na kusema: 'Tarehe 7 Novemba ilikuwa siku ya mwisho ya mwezi wa Dhul Qa'ada na kwa hivyo tarehe 8 Novemba ni siku ya kwanza ya Dhul Hija".
Kwa mujibu wa taarifa hiyo ya Ofisi ya Ayatullah Sistani tarehe 16 Novemba itakuwa siku ya Arafa na Jumatano tarehe 17 Novemba itasadifiana na 10 Dhul Hija ambayo ni siku ya Idul Adh'ha.
Aidha idara ya Darul Ifta ya Misri imetoa taarifa na kusema Novemba 8 ndio siku ya kwanza ya Dhul Hija na kutangaza kuwa sikukuu ya Idul Adh'ha itakuwa tarehe 17 Novemba.
691224