IQNA

Jarida la kielektroniki la Muungano wa Wanachuo wa Ulimwengu wa Kiislamu laanza kuchapishwa

13:35 - November 09, 2010
Habari ID: 2028706
Toleo la kwanza la jarida la kielektroniki la Thaqib limechapishwa mjini Tehran chini ya usimamizi wa sekretarieti ya Muungano wa Wanachuo wa Ulimwengu wa Kiislamu.
Jarida la kielektroniki la Thaqib linalochapishwa kwa lugha ya Kiarabu ni jarida la habari na uchambuzi linalochunguza na kujadili masuala na matatizo ya ulimwengu wa Kiislamu.
Mhariri mkuu wa jarida hilo la kila mwezi ni Ihsan Khosrojerdi. Timu ya jopo la wahariri wake inajumuisha Sayyid Ali Ridha Ahanchi, Muhammad Baqai, Mahdi Bahrami, Sayyid Muhammad Safavi, Fatima Ali Shah, Mussa Arabi na Muhammad Muhammadi.
Nakao makuu ya Muungano wa Wanachuo wa Ulimwengu wa Kiislamu yako mjini Tehran na jumuiya hiyo imekuwa na nafasi muhimu katika kutetea umma wa Kiislamu hususan wananchi wanaodhulumiwa wa Palestina. 691839

captcha