IQNA

Kamusi ya istilahi za Kiislamu na Kikristo kuchapishwa nchini Ujerumani

11:28 - November 11, 2010
Habari ID: 2029885
Kamusi ya istilahi za Kiislamu na Kikristo itachapishwa kwa lugha za Kituruki na Kijerumani kufikia mwaka 2012.
Kituo cha habari cha dw-world kimeripoti kuwa kamusi hiyo inatayarishwa na wanafikra wa Kiislamu na Kikristo wa Ujrumani kwa juhudi za Jumuiya ya Eugen Biser ya Munich. Inatazamiwa kuwa kamusi hiyo itachapishwa na kuingia sokoni mwishoni mwa mwaka 2012.
Lengo la kutayarishwa kamusi hiyo limetajwa kuwa ni kuimarisha uhusiano baina ya wafuasi wa dini za Kiislamu na Kikristo na kuwaelimisha wafuasi wa dini hiyo itikadi, fikra na mafundisho ya Kiislamu na Kikristo.
Kamusi hiyo inatayarishwa na mtaalamu wa lugha Mturuki na kundi la wahadhiri wa Kitivo cha Katoliki cha Chuo Kikuu cha Munich.
Mwaka 2005 Jumuiya ya Eugen Biser ilianzisha uhusiano wa kiutamaduni na kisayansi na kitivo cha Teolojia cha Chuo Kikuu cha Ankara na hadi sasa kumefanyika vikao kadhaa kati ya taasisi hizo mbili za kielimu kuhusu masuala mbalimbali. 693083
captcha