IQNA

Kitabu cha 'Mwamko wa Kiislamu katika Mtazamo wa Wamagharibi' chachapishwa Misri

12:33 - November 11, 2010
Habari ID: 2029913
Kitabu cha 'Mwamko wa Kiislamu katika Mtazamo wa Wamagharibi' kilichoandikwa na Muhammad Ammarah, mwandishi na mwanachama wa Jumuiya ya Utafiti wa Kiislamu ya al Azhar kimechapishwa nchini Misri.
Katika kitabu hicho mwandishi anachunguza sababu za kuenea satua na ushawishi wa dini ya Kiislamu kote duniani na wimbi kumbwa la kuingia kwenye dini hiyo tukufu wafuasi wa dini mbalimbali.
Mwandishi Muhammad Ammarah amechunguza na kujadili mustakbali wa mwamko wa Kiislamu katika jamii za Magharibi.
Mwandishi huyo wa Kimisri pia amechambua maudhui za kitabu hicho kwa njia za kiakili na kwa kuzingatia ukweli wa mambo na ametumia mitazamo na nadharia za wataalamu wa Magharibi wa masuala ya Mashariki katika kueleza mitazamo yake.
Kitabu cha 'Mwamko wa Kiislamu katika Mtazamo wa Wamagharibi' kimeandikwa kwa lugha ya Kiarabu na ndio toleo la hivi karibuni kabisa la machapisho ya Jumuiya ya Utafiti wa Kiislamu ya al Azhar.
Muhammad Ammarah, mwanafikra wa Kiislamu wa Misri na mwanachama wa Jumuiya ya Utafiti wa Kiislamu ya al Azhar alizaliwa mjini Cairo mwaka 1931. Ana shahada ya lugha ya Kiarabu na taaluma za Kiislamu na cheti cha uzamivu katika falsafa ya Kiislamu. 692830
captcha