Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Emarati WAM, Mkurugenzi wa Shirika la Kutengeneza Filamu la Anasy Bw. Anas Ghazal amesema filamu hiyo inalenga kuarifisha vazi la stara la wanawake Waislamu.
Amesema filamu hiyo itaangazia miundo mbalimbali ya vazi la Hijabu.
Ghazal ameendelea kusema kuwa shirika la Anasi lilianzishwa mwaka 2008 kwa lengo la kustawisha utamaduni na sana nchini Imarati. Ameongeza kuwa shirika hilo linapanga kuandaa tamasha na maonyesho ya vijana ili kuhimiza ubunifu. 694733