IQNA

Maonyesho ya Kimataifa ya Hija, Umra na Utalii wa Kiislamu kufanyika Indonesia

15:50 - November 14, 2010
Habari ID: 2031907
Maonyesho ya sita ya kimataifa ya Hija, Umra na Utalii wa Kiislamu yatafanyika tarehe 4 hadi 6 Februari katika mji mkuu wa Indonesia Jakarta yakiwashirikisha wawakilishi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Maonyesho hayo yatakayosimamiwa na Wizara ya Utamaduni na Utalii ya Indonesia yatafanya jitihada za kuimarisha sekta ya utalii wa Kiislamu, sekta ya mahoteli na hija na umra kwa kuwakutanisha pamoja maafisa na wawakilishi wa nchi za Kiislamu.
Maonyesho hayo yatawakutanisha pamoja maafisa wa sekta za utalii wa Kiislamu, wapangaji wa sera za hija na umra, waendeshaji wa masuala ya hoteli katika nchi za Kiislamu, wawekezezaji na wanunuzi kwa ajili ya kuimarisha mabadilishano ya kibiashara na kuzidisha uhusiano katika nyanja hizo.
Kandokando ya maonyesho hayo kutafanyika mkutano utakaojadili masuala mbalimbali yanayohusiana na hija, umra na utalii wa Kiislamu. 695157

captcha