Kwa mujibu wa tovuti ya maxihaber watazamaji wanaweza kuona matangazo hayo ya amali za hija mjini Makka, usomaji Qur'ani na ziara ya mahujaji mjini Madina kupitia anwani ifuatayo: www.kure.tv.
Lengo la televisheni hiyo kutangaza matangazo hayo kwa njia hiyo ni kuwawezesha Waislamu ambao hawakufanikiwa kuzuru miji hiyo mitakatifu kufuatilia kwa karibu ibada tukufu ya hija na ziara zinazofanywa na mahujaji katika miji hiyo.
Watu walio na hamu ya kunufaika na huduma za bure za televisheni hiyo wanaweza kufanya hivyo kupitia anwani iliyotajwa hapo juu au kupitia anwani ifuatayo ya simu ya mkononi: http://m.kure.tv. 695815