Baraza hilo limesema kuwa kupewa kibali cha kuitembelea Bahrain ujumbe huo ni udhalilishaji na dharau ya moja kwa moja kwa taifa la nchi hiyo na umma mzima wa Kiislamu.
Baraza hilo limesema kuwa kuruhusiwa ujumbe huo wa Kizayuni kuitembelea Bahrain ni dharau kwa damu ya maelfu ya mashihidi na wananchi madhlumu wa Palestina. Baraza hilo limeendelea kusema kuwa aina yoyote ile ya kuimarishwa uhusiano wa kidiplomasia na utawala haramu wa Israel pamoja na mashirika na makundi yanayounga mkono utawala huo ni jambo linalokwenda kinyume na matakwa ya mataifa ya Kiarabu na Kiislamu.
Huku likisisitiza kwamba mataifa hayo yanapinga vikali mazungumzo na mapatano ya aina yoyote yanayodhoofisha malengo matukufu ya taifa la Palestina, baraza hilo la wanazuoni wa Bahrain limesema kuwa watu wanaofuatilia kuboreshwa kwa uhusiano wa nchi za Kiarabu na utawala wa kigaidi wa Israel wanapaswa kutumia nguvu zao zote kwa lengo la kufanikisha malengo na thamani tukufu za Wapalestina. 696116