Maonyesho ya picha nadra za kale za al-Kaaba Tukufu na maeneo mengine matakatifu ya mji mtukufu wa Makka, picha ambazo zinarejea nyuma katika historia hadi karne ya 19 Milaadia, yanaendelea katika mji wa Dubai katika Umoja wa Falme za Kiarabu.
Maonyesho hayo yaliyopewa jina la ar-Ribh al-Khali ya mjini Dubai yataendelea hadi mwishoni mwa mwezi huu wa Dhul Hijja.
Picha hizo ambazo zinachukuliwa kuwa kongwe zaidi za mji mtakatifu wa Makka zilipigwa katika karne ya 19 na mtaalamu mmoja wa masuala ya Mashariki ya Kati raia wa Uholanzi. Wasimamizi wa maonyesho hayo wanasema kuwa watashirikiana na Chuo cha Leiden cha Uholanzi ili kukarabati hifadhi ya picha za mtaalamu huyo. 697032