Kwa mujibu wa gazeti la Al-Youm Al-Saba'a la Misri kongamano hilo litafanyika Jumapili tarehe 21 November katika Jumba la Makumbusho la Gayer-Anderson mjini Cairo.
Abul Ahmad Farghali Mkuu wa Kitengo cha Athari za Kiislamu cha Kitivo cha Akiolojia cha Chuo Kikuu cha Cairo anatazamiwa kuzungumza kuhusu uchoraji katika Uislamu wakati wa ufunguzi wa kikao hicho.
Kati ya masuala yatakayojadiliwa katika kongamano hilo ni mtazamo wa Uislamu kuhusu uchoraji, ubunifu wa Waislamu katika uchoraji na vilevile suala la 'Je Waislamu wa mwanzo walichora au la' litajadiliwa.
Kikao hicho pia kitaangazia ubunifu wa Waarabu na Waislamu katika sanaa ya uchoraji.
697936