Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Jumuiya ya Nchi za Kiislamu (ISESCO) linatayarisha hati mbili za Kiislamu zinazobeba anwani ya: "Mbinu za Sayansi, Falsafa, Fasihi na Sanaa kati ya Ulimwengu wa Kiislamu na Magharibi" na Ustaarabu wa Kiislamu katika Kioo cha Dunia, Upeo wa Falsafa".
Hati hizo mbili zitachapishwa kwa ushirikiano wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa UNESCO na Taasisi ya Muungano wa Tamadni.
Hati hizo zitajadili na kufanya mlingano kati ya mbinu za kisayansi, falsafa, fasihi na sanaa za ulimwengu wa Kiislamu na magharibi katika karne za 7 hadi 9 Miladia.
Siku chache zilizopita pia UNESCO ilisimamia mkutano wa Farabi na Harakati ya Mwamko wa Ulaya. Mkutano huo ulifanyika katika makao ya shirika hilo mjini Paris, Ufaransa. 698699