IQNA

Hatua ya mwisho ya mashindano ya Qur'ani ya Dubai kufanyika mwezi Januari mwakani

18:52 - November 23, 2010
Habari ID: 2036887
Hatua ya mwisho ya awamu ya 12 ya mashindano ya kitaifa ya kuhifadhi Qur'ani Tukufu nchini Imarati, imepangwa kufanyika tarehe 22 hadi 31 Januari mwakani.
Kwa mujibu wa tovuti ya Tuzo ya Dubai, Habari hiyo imetangazwa na Ibrahim Muhammad, mkuu wa kamati inayosimamia mashindano hayo ambaye pia ni mshauri wa masuala ya kiutamaduni wa Amir wa Dubai.
Hatua ya mwanzo ya mashindano hayo itafanyika katika miji tofauti ya Umoja wa Falme za Kiarabu tokea tarehe 2 hadi 11 Disemba, ambapo washindi wa hatua hiyo wataruhusiwa kuingia katika hatua ya pili. Mashindano mengine ya al-Hafidh al-Muwatin ambayo huandaliwa kila mwaka na Taaisi ya Kimataifa ya Qur'ani ya Dubai yatafanyika katika mji huo tarehe 28 mwezi huu wa Novemba. Akizungumzia suala hilo Ahmad Swafar as-Suweidi mwanachama wa kamati inayoandaa mashindano hayo amesema kuwa suhula zote zinazohitajika zimeandaliwa kwa ajili ya kuyafanikisha. 700327
captcha