IQNA

OIC yalaani njama za utawala wa Kizayuni za kuharibu al Aqsa

9:22 - November 27, 2010
Habari ID: 2037686
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiislamu OIC Profesa Ekmeleddin Ihsanoglu ametoa taarifa akiulani vikali Utawala wa Kizayuni wa Israel kwa kuendeleza njama zake za kuharibu Quds Tukufu.
Katika taarifa hiyo Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiislamu amesema kile kinachofanywa na utawala haramu wa Israel katika Quds Tukufu ni ukiukwaji wa wazi wa sheria za kimataifa.
Profesa Ekmeleddin Ihsanoglu ameonya kuhusu hatari zinazoukabili Msikiti wa Al Aqsa na maeneo ya kihistoria pembizoni mwake. Katibu Mkuu wa OIC ameutaka utawala haramu wa Israel kusitisha mara moja operesheni zake haribifu zenye lengo la kubadilisha muundo wa Kiislamu, Kikristo na Kipalestina wa Quds Tukufu.
Hivi karibuni Mufti wa Quds alitahadharisha juu ya njama za utawala wa Kizayuni wa Israel za kutaka kuuyahudisha mji mtakatifu wa Quds. Sheikh Muhammad Hussein alisema kwamba, hatua ya utawala wa Kizayuni wa Israel ya kuchimba mashimo ya chini kwa chini katika msikiti wa al-Aqsa na kuendeleza ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni ina lengo la kubadilisha muundo wa kijamii na kijiografia wa mji wa Quds.
Mufti Muhammad Hussein alitoa wito kwa nchi za Kiislamu kuchukua hatua ambazo zitaufanya utawala huo ghasibu usitishe hatua zake hizo za kuuyahudisha mji mtakatifu wa Quds.
701676
captcha