Baraza hilo limelitaka Bunge la Ufaransa kubuni kamati ya kuchunguza kwa kina kitendo cha kukosewa heshima maeneo ya ibada na Kiislamu ya Ufaransa pamoja kuandikwa maandishi ya kibaguzi kwenye milango ya msikiti huo.
Katika sehemu nyingine ya taarifa hiyo, Baraza la Waislamu wa Ufaransa limebainisha wasiwasi wake mkubwa kuhusiana na kuongezeka kwa vitendo vya dharau dhidi ya maeneo ya ibada na kidini nchini Ufaransa na kutaka vyombo vya serikali vichukue hatua madhubuti za kukabiliana na vitendo hivyo vinavyovuruga umoja na mshikamano wa kitaifa.
Licha ya kuungana na Waislamu wa mji wa Marmande katika kulaani kitendo hicho cha dharau, baraza lililotajwa limewataka Waislamu wa nchi hiyo kuwa watulivu katika kukabiliana na kitendo hicho cha dharau dhidi ya matukufu yao.
Jumamosi iliyopita watu wasiojulika waliandika maandishi ya kibaguzi na dharau na vilevile kuchora michoro ya msalaba kwenye milango na kuta za msikiti wa mji wa Marmande. Pia waliandika majina ya Lut na Qaroon kwenye mlango wa kuingilia wanawake kwenye msikiti huo. 703109