Kituo cha habari cha Chuo Kikuu cha Tehran kimeripoti kuwa kongamano hilo linafanyika kwa kutilia maanani nafasi aali ya Sheikh Shahabuddin Yahya Suhrawardi mbaye ndiye muasisi wa Falsafa ya Ishraq (falsafa ya mnururisho) katika ulimwengu wa Kiislamu.
Kwa mujibu wa kituo hicho, kongamano hilo litasimamiwa na Chuo Kikuu cha Tehran na Taasisi ya Utafiti wa Falsafa ya Iran kwa ushirikiano wa Chuo Kikuu cha Damascus na Chuo Kikuu cha Halab kuanzia tarehe 22 hadi 24 Februari. 704518