Kwa mujibu wa gazeti la al-Jazeera linalochapishwa nchini Kuwait Khalid Abu Gheit, mkuu wa idara inayoshughulikia masuala ya Qur'ani katika Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu ya Kuwait, akizungumza katika sherehe ya ufunguzi wa kituo hicho amesema kuwa Taasisi ya Kuhifadhi Qur'ani ya as-Shatibi imekuwa na nafasi muhimu katika kulea kizazi cha wahifadhi Qur'ani Tukufu. Ameelezea matumaini yake kwamba taasisi hiyo itafanikiwa kufikisha vituo vyake vya kuhifadhi Qur'ani hadi 70.
Akizungumza katika sherehe hiyo Amal Saidi, mkuu wa kituo hicho kipya cha wanawake amesema kuwa kutoa mafunzo bora ya kuhifadhi Qur'ani, kuwasaidia wasomi na wahifadhi Qur'ani, kubainishiwa wanawake mafundisho halisi ya Qur'ani Tukufu na kuimarisha thamani za Qur'ani katika matabaka mbalimbali ya jamii ni baadhi ya malengo ya kituo hicho. Amesema kituo hicho kitawakubali wanafunzi wa kike walio na umri wa kati ya miaka minane hadi 60. 705526