IQNA

Waturuki wavutiwa na maonyesho ya 'picha za Ashura'

13:49 - December 04, 2010
Habari ID: 2041556
Maonyesho ya 'picha za Ashura' yaliyoanza siku ya Alkhamisi katika Kituo cha Utamaduni cha Cem Karaca katika eneo la Bakirkoy mjini Istanbul yamewavutia wananchi wengi wa Uturuki.
Kwa mujibu wa tovuti ya Zeinabiyya ya mjini Istanbul maonyesho hayo yamedhaminiwa na Jumuiya ya Mashia wa Ithna Asheri wa Uturuki kwa ushirikiano wa meya wa Istanbul kwa lengo la kuonyesha picha za maombolezo yanayofanywa na Mashia kwa ajili ya kukumbuka kuuawa shahidi Imam Hussein (as), mjukuu mpenzi wa Mtume Muhammad (saw). Waliohudhuria sherehe ya ufunguzi wa maonyesho hayo ni pamoja na Sinan Kilic, mkuu wa jumuiya iliyotajwa, Hamit Turan, imamu wa swala ya jamaa wa Msikiti wa Zeinabiyya wa Istanbul pamoja na idadi kubwa ya wanazuoni wa Kishia na wapenzi wa Watu wa Nyumba ya Mtume (saw).
Wageni wanaotembelea maonyesho hayo pia wamepewa fursa ya kuandika na kudhihirisha maoni yao kuhusiana na tukio zima la Ashura na shakhsia ya Shahid Imam Hussein (as) katika daftari maalumu lililotayarishwa kwa lengo hilo.
Tunakumbusha hapa kuwa sehemu ya kwanza ya maonyesho hayo ilifanyika tarehe 22 hadi 30 Novemba katika Kituo cha Utamaduni cha Bulent Ecevit mjini Istanbul. 705610
captcha