Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, kitabu hicho chenye kurasa 213 kina dibaji iliyoandikwa na Sheikh Hamidou Kane, mhadhiri wa Uislamu na Masomi ya Kijamii nchini Senegal na kimechapishwa na Shirika la Uchapishaji la Silex-Nouvelles du Sud.
Mwandishi anasisitiza katika kitabu hicho kuwa kuna haja ya kuwepo mazungumzo baina ya tamaduni na kuandika: "Mazungumzo baina ya tamaduni na dini ni hitajio la kihistoria ambalo linapaswa kulenga nukta za pamoja badala ya tofauti ingawa misingi ya kiutamaduni ya kila jamii inapaswa kuheshimiwa".
Katika utangulizi wake Sheikh Hamidou Kane anaandika kuwa yeye kama walivyo wakaazi wengine wa Senegal na nchi za Afrika, anaishi katika eneo lenye aina mbalimbali za lugha na tamaduni na ndio sababu kitabu chenye maudhui muhimu kama hiyo kimeandikwa.
705513