Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Jumuiya ya Nchi za Kiislamu ISESCO na Jumuiya ya Kimataifa ya Familia zimetiliana saini hati ya ushirikiano katika kikao kilichofanyika Paris, Ufaransa.
Katibu Mkuu wa ISESCO Abdul Aziz al Tuwaijri ambaye amehutubia kikao cha Jumuiya ya Kimataifa ya Familia (OMF) kama mgeni wa heshima, alikutana na kufanya mazungumzo na Mwenyekiti wa shirika hilo.
Pande hizo mbili zilitia saini hati ya ushirikiano katika masuala ya elimu, familia na kuboresha uhusiano, haki za binadamu na mazungumzo kati ya tamaduni mbalimbali na zimesisitiza juu ya udharura wa kupambana na umaskini na kutayarisha mazingira ya kutambuana kwa tamaduni mbalimbali kupitia vitabu vya masomo.
Kikao cha kimataifa cha familia kilifanyika tarehe 3 hadi 5 Disemba mjini Paris. Katibu Mkuu wa ISESCO ambaye alihutubia kikao hicho amesisitiza juu ya umuhimu wa nafasi ya familia katika kulea kizazi cha mwanadamu. 707431