IQNA

Chuo cha kidini cha al-Ghadir chafunguliwa Bahrain

16:56 - December 07, 2010
Habari ID: 2043976
Chuo cha kidini cha al-Ghadir kimefunguliwa katika mji wa Sitra nchini Bahrain kwa kuhudhuriwa na ujumbe wa Baraza la Maulama wa Kishia la Bahrain.
Kwa mujibu wa tovuti ya baraza hilo, wanachama wa baraza hilo, wahadhiri na wanachuo wa chuo hicho wamehudhuria sherehe ya kufunguliwa chuo hicho.
Chuo cha kidini cha al-Ghadir ambacho kimeanzishwa chini ya uenyekiti wa Sheikh Abdul Hussein Satri na usimamizi wa Hujjatul Islam wal Muslimin Ibrahim Swafa kitaendeshwa kwa ushirikiano wa wahadhiri mashuhuri wa masuala ya kidini kwa lengo la kulea na kutoa mafunzo ya kidini kwa wanafunzi walio na hamu ya kunufaika na masomo hayo. 708134
captcha