Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Malaysia la Bernama, Waziri Mkuu Najib amesema kuna makundi ambayo yamefanikiwa kutumia vyombo vya habari kwa makusudi na mpangilio maalumu kueneza propaganda chafu dhidi ya Uislamu.
"Tatizo hilo ni sugu hasa wakati propaganda zinapofanikiwa na watu wanaanza kuuchukia Uislamu. Hali hii ya kusikitisha inatokana na Waislamu kushindwa kutumia vyombo vya habari kusahihisha taswira potofu inayoenezwa kuhusu Uislamu", amesema Waziri Mkuu wa Malaysia wakati wa kuzinduliwa Televisheni ya kwanza ya Kiislamu ya nchi hiyo, TV Al Hijrah' mjini Kuala Lumpur.
Najib ameongeza kuwa ni Waislamu wachache wanaomiliki vyombo vya habari na kwamba ukosefu wa ubunifu katika kanali za televisheni za Kiislamu ni jambo ambalo limefanya kizazi cha vijana kutozitazama.
708916