Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, kitabu hiki chenye kurasa 84 kimeandikwa na Hassan Kadhim Al Fatal, malenga na mwanafasihi Muiraqi.
Hassan Kadhim Al Fatal amesema kuwa kitabu hicho kina kurasa tatu na kwamba sura ya kwanza inaeleza umuhimu, fadhila na faida za ziyara ya Imam Hussein AS, nayo sura ya pili inachunguza malengo na sababu za harakati ya Imam Hussein AS huku sura ya tatu ikichunguza umuhimu wa kufanya majlisi za kuomboleza tukio la kuuawa shahidi Imam Hussein AS.
Hussein Kadhim al Fatal alizaliwa mwaka 1952 katika mji mtakatifu wa Karbala na ni mwanachama wa jumuiya ya malenga wa Kiarabi na mwanachama wa Jumuiya ya Radio na Televisheni Iraq.
708892