IQNA

Filamu ya 'Maafa kutoka Gaza' yashinda tuzo ya filamu ya Ufaransa

17:07 - December 11, 2010
Habari ID: 2046060
Filamu ya Maafa kutoka Gaza, Siku Inayofuata" (Gaza-Strophe, le jour d’après) iliyotengenezwa na Samir Abdullah na Khairuddin Mabruk imeshinda tuzo ya filamu bora zaidi matukio ya kweli ya tamasha ya Tuzo ya Kimataifa ya Filamu za Matukio ya Kweli na Ripoti ya Meaditerania" iliyofanyika katika mji wa Marseille nchini Ufaransa.
Kituo cha habari cha Saphirnews kimeripoti kuwa filamu hiyo inaonyesha picha za mashambulizi ya utawala wa Kizayuni wa Israel huko Gaza na hatima ya wananchi Waislamu wa eneo hilo baada ya kumalizika vita hivyo vya maangamizi.
Jopo la majaji wa tamasha hilo limesema kuwa filamu hiyo ilimestahiki kupata tuzo bora ya filamu za matukio ya kweli (documentary) kutokana na kuonyesha vyema picha za matukio ya Mashariki ya Kati na kutayarisha uwanja mzuri wa kuelewa hali ya sasa ya eneo hilo.
Ni vyema kukumbusha hapa kuwa filamu hiyo ya matukio ya kweli kuhusu vita vya Gaza ilionyeshwa kwa mara ya kwanza katika kanali ya televisheni ya France ô na itaanza kuonyeshwa kwa watu wote mwanzoni mwa mwaka ujao.
Mtayarishaji wa filamu hiyo Samir Abdullah amesema kuwa tuzo hiyo kwa hakika ni zawadi ka mapambano ya wananchi wa Palestina na uungaji mkono kwa wanamapambano ambao wanafanya juhudi za kulinda utambulisho wao mkabala wa tingatinga za mauaji za utawala ghasibu wa Israel unaotaka kuwaangamiza. 710375
captcha