Mafunzo hayo ambayo yanadhaminiwa na Idara ya Wakfu na Masuala ya Misikiti ya al-Uneiza yana lengo la kunyanyua kiwango cha elimu cha maimamu na waadhini wa misikiti.
Kuhusu jambo hilo, Fahd al-Khalifa mkuu wa idara hiyo amesema, mafunzo ya fiqhi kwa maimamu na waadhini kwa shabaha ya kupambana na fikra potofu na kutafutwa njia za kuimarisha ushirikiano kati ya wakuu wa idara hiyo na maimamu wa misikiti ni lengo kuu la kuendeshwa masomo hayo ya muda mfupi.
Mwakilishi wa Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu na Tablighi ya Saudi Arabia atasimamia uendeshwa wa masomo hayo. 710225