IQNA

Wakuu wa Maktaba za Kiislamu kukutana Cairo

8:46 - December 12, 2010
Habari ID: 2046178
Kongamano la Kwanza la Wakuu wa Maktaba za Vyuo Vikuu vya Nchi za Kiislamu kitafanyika Cairo kuanzia Disemba14-16 katika Chuo Kikuu cha Cairo nchini Misri.
Kwa mujibu wa tovuti ya Shirika la Nchi za Kiislamu la Elimu, Sayansi na Utamaduni ISESCO, kongamano hilo litafanyika kwa ushirikiano na Chuo Kikuu cha Cairo, ISESCO na Umoja wa Vyuo Vikuu vya Kiislamu FUIW. Mada kuu ya kikao hicho itakuwa "Kuelekea katika Muungano wa Kimfumo kwa ajili ya Kujenga Jamii za Kisayansi".
Kongamano hilo ni sehemu ya juhudi za ISESCO na Umoja wa Vyuo Vikuu vya Kiislamu za kuimarisha utamaduni wa mazungumzo na amani.
Washiriki wa kongamano hilo ni kutoka maktaba za vyuo vikuu vya Bahrain, Misri, Jordan, Iraq, Kuwait, Libya, Morocco, Nigeria, Saudi Arabia, Qatari, Syria , Sudan na Yemen.
710291
captcha